Unapenda Upweke au Unapenda Amani?

Mara nyingi tunajitambulisha kama “watu wa ndani (introverts)” kwa sababu tunapenda kuwa peke yetu. Lakini ukweli ni kwamba, si kila anayependa upweke ni introvert. Wengine wanapenda upweke kwa sababu humo ndiko wanakopata amani ya ndani.

Quote ya leo inatufundisha:

“Unadhani wewe ni mtu wa ndani kwa sababu unapenda kuwa peke yako.
Lakini kwa uhalisia unapenda kuwa na amani.
Na ukweli ni kwamba wewe ni mchangamfu unapokuwa na watu wanaokuletea amani.”

Hii inatufunza kuwa utu wetu wa kijamii unategemea mazingira na watu tunaoshirikiana nao. Si kwamba tunachukia watu, bali tunachagua wale wanaoongeza thamani, furaha na utulivu kwenye maisha yetu.

Kisaikolojia, hii ni kanuni ya msingi ya mahusiano ya kibinadamu: Tunachanua zaidi tunapokuwa karibu na watu tunaohisi usalama na amani.


Changamoto ya Leo:
Je, wewe hujisikiaje unapokuwa na watu wanaokuletea amani? Na ni akina nani hao katika maisha yako?


Mwisho:
Chagua kuwa karibu na watu wanaoleta amani, si vurugu. Utajikuta wewe mwenyewe ukiwa wa furaha na mchangamfu zaidi. 🌿

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top